Andrea Bessette
From Wikipedia, the free encyclopedia
Andrea Bessette (maarufu kama Frère André; Mont-Saint-Grégoire, 9 Agosti 1845 – Montréal, 6 Januari 1937), alikuwa bradha wa shirika la Msalaba Mtakatifu nchini Kanada.
Alizaliwa katika familia ya kawaida yenye watoto wengi, akawahi kubaki yatima na kukabidhiwa kwa utunzaji wa shangazi. Alifanya kazi katika kiwanda cha nguo huko Kanada na Marekani .
Mwaka 1870 aliingia utawani akapewa kazi ya bawabu wa ofisi ya chuo cha Notre-Dame huko Montreal.
Alikuwa na sifa kama mponyaji [1].
Alithibitishwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri mnamo 1982, Papa Benedikto XVI akamtangaza mtakatifu tarehe 17 Oktoba 2010.