Ziwa Vostok
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ukweli wa haraka
| |
Nchi zinazopakana | Antaktiki |
Eneo la maji | km2 12,500 |
Kina cha chini | mita 432 |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
,ita -500 |
Funga
Ziwa Vostok ni ziwa lililopo kwenye Bara la Antaktiki chini ya ngao ya barafu. Ni moja kati ya maziwa 400 yaliyotambuliwa chini ya barafu ya Antaktiki; ni ziwa kubwa la bara hilo.
Ni ziwa lenye maji ya kumiminika yaliyo mita 4000 chini ya uso wa barafu ya Antaktiki.
Jina lake limetokana na Kituo cha Vostok cha Urusi kilichopo kwenye uso wa barafu juu yake.
Kuwepo kwa ziwa hilo liligunduliwa na wanasayansi wa Urusi na Uingereza waliotumia mitambo ya rada.
Ziwa lina maji safi. Jotoridi ya maji ni karibu -3 °C lakini hayagandi, hubaki kiowevu kwa sababu ya shinikizo kubwa la barafu juu yake.