Uingereza (maana)
ukarasa wa maana wa Wikimedia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Uingereza ni neno linaloweza kutaja maana mbalimbali:
- nchi ya Uingereza (England) katika kusini ya kisiwa cha Britania ambayo ni sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini
- Kisiwa cha Britania (Great Britain) ambacho ni kisiwa kikubwa cha Ulaya chenye nchi tatu za Uingereza, Uskoti na Welisi
- dola la Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland)
- kihistoria ufalme wa Uingereza katika nchi hii hadi kuunganishwa na Uskoti mwaka 1701
- Milki ya Kiingereza iliyojumlisha Ufalme wa Muungano na koloni zake kote duniani
- katika lugha ya kila siku maana yoyote iliyotajwa hapo juu
- Redio Tanzania imependekeza neno moja la "Uingereza“ kwa ajili ya maana yote tatu
- TUKI imependekeza maneno mawili ya Uingereza (kwa nchi pia kwa ajili ya Ufalme wa Muungano) na Briteni (kwa ajili ya kisiwa); lakini "Briteni“ ina matatizo kwa maandishi ya kihistoria na kijiografia kwa sababu inafanana mno na jina la "Brittany“ au "Bretagne“ amabyo ni mkoa wa Ufaransa.
- BAKITA lilipendekeza 'Inglandi' kwa ajili ya England; ila inasema kwamba haitumiki sana
- Makala hii inajaribu kutumia neno la "Britania“ na kusubiri michango ya wanawikipedia.
Ukurasa huu una maelezo ya maana ili kutofautisha nia mbalimbali zinazolengwa na neno moja. Kwa usaidizi kuhusu makala za aina hii tazama Msaada:Maana
Maelezo katika ukurasa huu yawe mafupi, na kwa kila maana kuwe na kiungo kimoja tu ambacho kiunge ukurasa kuhusu nia yenye maana hii. Ukiwa umefika hapa kwa kutumia kiungo katika makala nyingine, tafadhali badalisha kiungo kile kiunge makala iliyokusudiwa moja kwa moja. |