Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1972
From Wikipedia, the free encyclopedia
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1972 ulikuwa wa 47 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 7 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rais Richard Nixon (pamoja na kaimu wake Spiro Agnew) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" George McGovern (pamoja na kaimu wake Sargent Shriver).