Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1968
From Wikipedia, the free encyclopedia
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1968 ulikuwa wa 46 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 5 Novemba. Upande wa "Republican Party", mgombea Richard Nixon (pamoja na kaimu wake Spiro Agnew) aliwashinda mgombea wa "Democratic Party" Hubert Humphrey (pamoja na kaimu wake Edmund Muskie) na mgombea wa "American Independent Party" George Wallace (pamoja na kaimu wake Curtis LeMay).