Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1956
From Wikipedia, the free encyclopedia
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1956 ulikuwa wa 43 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 6 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rais Dwight Eisenhower (pamoja na kaimu wake Richard Nixon) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" Adlai Stevenson II (pamoja na kaimu wake Estes Kefauver).