Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1864
From Wikipedia, the free encyclopedia
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1864 ulikuwa wa 20 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 8 Novemba. Upande wa "Republican Party" (chini ya jina la "National Union"), Rais Abraham Lincoln (pamoja na kaimu wake Andrew Johnson) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" George McClellan (pamoja na kaimu wake George Pendleton).