Tumbusi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tumbusi au tai mzoga ni ndege wakubwa wa nusufamilia Aegypiinae na Gypaetinae katika familia Accipitridae ambao hula mizoga. Wana mnasaba na tai. Huko Amerika kuna ndege wafananao na tumbusi, lakini wale hawana mnasaba sana na huwekwa katika familia Cathartidae. Tumbusi huvumbua mizoga kwa macho, lakini wale wa Marekani wananusa vizuri pia.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Tumbusi | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Tumbusi uso-njano | ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusufamilia 2, jenasi 9 za tumbusi:
| ||||||||||
Funga
Spishi nyingi za tumbusi zina kichwa bila manyoya. Sifa bainifu hii imekua kuzuia manyoya ya kichwa yasichafuliwe kwa damu wakati tumbusi akiingiza kichwa chake ndani ya mzoga. Kichwa chenye upara kinaweza kusafishwa kwa urahisi ndani ya mto au ziwa.