Tiketi
ukarasa wa maana wa Wikimedia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Tiketi (pia: tikiti, kutoka Kiingereza "ticket") ni kipande cha karatasi au kadi inayoidhinisha mtu kuingia, kushiriki, kutumia au kusafiri. Tiketi huuzwa moja kwa moja au kidijitali siku ya matumizi au siku kadhaa kabla ya siku ya matumizi kufika.
Tiketi nyingine hushindaniwa au kutolewa bure kwa washiriki wakitimiza yanayohitajika au kama zawadi mtu anaponunua kitu au kulipa huduma fulani.