Tassili n'Ajjer
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tassili n'Ajjer ni safu ya milima katika Jangwa la Sahara nchini Aljeria. Kutokana na mimea iliyoweza kudumu hapa imetambuliwa kama hifadhi ya bioanwai. Kuna pia michoro mingi ya miambani kutoka enzi ya historia ya awali. Eneo lote limekuwa hifadhi ya kitaifa na kupokewa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.