Robben Island
From Wikipedia, the free encyclopedia
Robben Island ni kisiwa kidogo 12 km mbele ya mji wa Cape Town (Afrika Kusini) katika Atlantiki. Kisiwa kina eneo la hektari 547, urefu ni km 4.5 na upana hadi km 1.5.
Kisiwa kimejulikana kutokana na gereza lake na mfungwa mashuhuri Nelson Mandela. Wafungwa pamoja naye walikuwa Walter Sisulu, Govan Mbeki na Robert Sobukwe.
Siku hizi kisiwa ni makumbusho na hifadhi ya mazingira. Watumishi wanaotembeza wageni ni wafungwa wa zamani.
Kipo kwenye orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.