Puebla (jimbo)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Puebla ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kati-mashariki ya nchi. Mji mkuu na mji mkubwa ni Puebla.
Imepakana na Veracruz, Hidalgo, Mexico (jimbo), Tlaxcala, Guerrero, Morelos na Oaxaca.
Kunako mwaka wa 2005, idadi ya wakazi ilikuwa 5,383,133. Una eneo la 33,902 km².
Jina lake limetokana na jina la mji wa Puebla (jina rasmi: La Puebla de los Angeles; kiswahili: mji wa malaika).
Gavana wa jimbo ni Mario Marín Torres.
Lugha rasmi ni Kihispania.