Orodha ya departements za Ufaransa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Departement ni kitengo cha utawala nchini Ufaransa. Inalingana na ngazi ya wilaya. Departement inaongozwa na mkuu wake ambaye kwa lugha ya Kifaransa anaitwa prefect.
Kwa jumla kuna wilaya 101 za aina hii. Hizi zimepangwa katika mikoa (region) 18.
Kati yake, departement 96 tu ziko Ufaransa bara na kisiwa jirani cha Corsica, nyingine 5 ziko nje ya Ulaya ambako wakazi wa yaliyokuwa makoloni waliamua kubaki sehemu za Ufaransa na maeneo hayo kupewa hadhi ya departement, wakati huohuo ni pia mikoa. Hizi departments za ng'ambo ni: Guadeloupe na Martinique katika Karibi, Guayana katika Amerika Kusini, Réunion na Mayotte) kwenye bahari Hindi.