Nyanda za juu za Brazil
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nyanda za juu za Brazil (kwa Kireno: Planalto Brasileiro) ni eneo kubwa katika mashariki, kusini na katikati ya Brazil. Eneo lake ni kama theluthi ya nchi yote na sehemu kubwa ya watu wa Brazil (190,755,799; sensa ya 2010) wanaishi katika nyanda za juu au kwenye kanda nyembamba ya pwani iliyopo kati ya bahari na milima hiyo.