Mbuzi-kaya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mbuzi-kaya ni mnyama katika ngeli ya mamalia ambaye huzaa na kunyonyesha mwenye miguu minne na mwenye tabia zinazofanana na ng'ombe. Kwa ukubwa, mbuzi aliyekomaa ni pungufu ya theluthi moja ya ng'ombe aliyekomaa.
Mbuzi-kaya | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mbuzi na mwanawe | ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Mbuzi-kaya, kama alivyo n'gombe, ni mnyama anayefugika. Hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa na ngozi yake. Kwani nyama na maziwa ni chakula, na ngozi kufanywa viatu, mishipi na mikoba pia.
Mbuzi-kaya hula majani, hucheua na kutafuna tafuna chakula chake mara kadhaa ilhali kikizunguka kati ya vyumba mbalimbali vya tumbo na mdomo wake kabla ya kukimeza kabisa, kama vile afanyavyo ng'ombe.
Mara nyingi mbuzi-kaya hubeba mimba na kuzaa mapacha kadhaa.
Mbuzi ni kati ya wanyama wa kwanza waliofugwa na binadamu. Kuna spishi za kufugwa na spishi za porini.