Lahn
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mto Lahn ni tawimto la Rhine nchini Ujerumani. Una urefu wa kilomita 245 ukipita kwenye majimbo ya shirikisho ya Rhine Kaskazini-Westfalia (km 23.0 ), Hesse (km 165.6), na Rhine-Palatino (km 57.0).
Chanzo chake kiko kwenye milima ya Rothaargebirge ukiishia kwenye mto Rhine huko Lahnstein, karibu na Koblenz.
Miji muhimu kando ya Lahn ni pamoja na Marburg, Gießen, Wetzlar, Limburg an der Lahn, Weilburg na Bad Ems.