Msumbiji (kisiwa)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kisiwa cha Msumbiji (kwa lugha ya Kireno: "Ilha de Moçambique") ni kisiwa kidogo (na pia mji) kilichopo km 3 mbele ya mwambao wa Msumbiji ya kaskazini. Urefu ni km 3 na upana kati ya m 500 hadi 200. Kisiwa ni sehemu ya mkoa wa Nampula.
Kisiwa kilikuwa chanzo cha koloni la Kireno la Msumbiji na mji ulikuwa mji mkuu wa nchi kwa karne kadhaa hadi mwaka 1898 BK. Leo hii mji umepanuka kote kisiwani. Kuna wakazi 60,000 wanaoishi katika mji wenye sehemu mbili: mji wa mawe upande wa kaskazini na mji wa makuti upande wa kusini.