Kifutio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kifutio au raba (kutoka Kiingereza rubber) ni kifaa kinachotumiwa kufuta alama za penseli au aina za kalamu. Kimsingi ni kipande kigumu cha mpira kinachotumiwa kufutia maandishi.
Mara nyingi kipande kidogo cha mpira kimefungwa kwenye penseli yenyewe wakati inapotengenzwa. Ilhali vipande vidogo huisha haraka au kuvunjika ni afadhali kuwa na kipande kikubwa.
Ziko aina tofauti hasa katika kiwango cha ugumu; tofauti nyingine ni uundaji kutokana na utomvu wa mpira au plastiki.