Karen Blixen
Mwandishi wa Denmark / From Wikipedia, the free encyclopedia
Karen Christence Blixen-Finecke (jina la kiuandishi alilotumia kwenye nchi zinazozungumza Kiingereza: Isak Dinesen) (Rungsted/ Denmark 17 Aprili 1885 - 7 Septemba 1962) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Alitumia pia majina ya Tania Blixen, kwenye nchi zinazozungumza Kijerumani, Osceola na Pierre Andrézel.
Aliishi Kenya -wakati ule: Afrika ya Mashariki ya Kiingereza- kati ya 1913 hadi 1931 akiongoza shamba la kahawa karibu na mji wa Nairobi. Eneo la shamba lake la zamani hadi leo laitwa "Karen" ni kitongoji cha Nairobi.
Aliandika kumbukumbu ya maisha yake Kenya na kitabu hiki kikawa msingi wa filamu "Out of Africa". Huko Denmark alijulikana sana kwa kazi yake iitwayo Seven Gothic Tales.