Go-Fushimi wa Japani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Go-Fushimi (5 Aprili, 1288 ā 17 Mei, 1336) alikuwa mfalme mkuu wa 93 (Tenno) wa Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Tanehito, na alikuwa mwana wa kwanza wa Tenno Fushimi. Mwaka wa 1298 alimfuata babake, na kuwa mfalme hadi kujiuzulu 1301. Aliyemfuata kama Tenno ni binamu yake Go-Nijo.