Frankfurt am Main
From Wikipedia, the free encyclopedia
Frankfurt am Main ni kati ya miji mikubwa ya Ujerumani. Ina wakazi 747,000. Rundiko la mji wa Frankfurt pamoja na miji mingine kama Mainz na Wiesbaden inaitwa eneo la Rhein-Main lenye wakazi milioni nne.
"Frankfurt" inaelekezwa hapa. Kwa matumizi mengine, tazama Frankfurt (maana).
Ukweli wa haraka Nchi, Jimbo ...
Frankfurt am Main | |
Mahali pa mji wa Frankfurt am Main katika Ujerumani |
|
Majiranukta: 50°6′37″N 8°40′56″E | |
Nchi | Ujerumani |
---|---|
Jimbo | Hesse |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 746.878 |
Tovuti: www.frankfurt.de |
Funga
Frankfurt ni kitovu cha uchumi ch Ujerumani hasa makao makuu ya benki kubwa. Uwanja wa Ndege wa Rhein-Main ni mkubwa katika Ujerumani. Barabara kuu na njia kuu za reli za Ujerumani hukutana hapa.
Frankfurt ni makao makuu ya Benki Kuu ya Ulaya na Benki Kuu ya Ujerumani.
Mji umekuwa na tabia ya kimataifa. Takriban kila mkazi wa tatu ana asili yake nje ya Ujerumani.