Dameski
From Wikipedia, the free encyclopedia
Dameski (pia: Damasko, Damaskus, Damascus; kutoka Kiarabu: دمشق "dimashk") ni mji mkuu wa Syria, pia ni mji mkubwa wa nchi hiyo wenye wakazi milioni 2, wanaofikia 5 pamoja na miji jirani.
Ukweli wa haraka Habari za msingi, Lage ...
Mkoa | Dameski |
Anwani ya kijiografia | 33°30'35" N; 36°18'33"E |
Kimo | 690 m juu ya UB |
Eneo | 105 km² |
Wakazi | 1.711.000 (2009) |
Msongamano wa watu | watu 15.056/km² |
Simu | 963 (nchi), 11 (mji) |
Lage | |
Funga
Dameski ni kati ya miji ya kale kabisa duniani iliyoendelea kukaliwa mahali palepale: inaaminiwa imekaliwa tangu miaka 8,000 au zaidi.
Mji wa Kale umo katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.