Bosnia na Herzegovina
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bosnia na Herzegovina (Bosna i Hercegovina au Босна и Херцеговина) ni nchi ya Ulaya kusini mashariki kwenye rasi ya Balkani. Mara nyingi huitwa kwa kifupi "Bosnia" tu na watu wake "Wabosnia". Ilikuwa sehemu ya Yugoslavia hadi mwaka 1992.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: "Intermeco" | |||||
Mji mkuu | Sarajevo 43°52′ N 18°25′ E | ||||
Mji mkubwa nchini | Sarajevo | ||||
Lugha rasmi | Kibosnia, Kikroatia, Kiserbia | ||||
Serikali Marais Mwenyekiti wa halmashauri ya mawaziri |
Jamhuri Šefik Džaferović (Mbosnia) Milorad Dodik 1(Mserbia) Željko Komšić (Mkroatia) Zoran Tegeltija | ||||
Uhuru Ilitambuliwa |
6 Aprili 1992 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
51,197 km² (128) -- | ||||
Idadi ya watu - Julai 2006 kadirio - 2014 sensa - Msongamano wa watu |
4,498,9762 (ya 1273) 3,871,643 76/km² (ya 1163) | ||||
Fedha | Convertible mark pamoja na Euro ( BAM4 ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .ba | ||||
Kodi ya simu | +387
- | ||||
1 Maraisi watatu wanaobadilishanan 2 Kadirio ya CIA World Factbook . |
Eneo lake ni km² 51,129 linalokaliwa na wakazi karibu milioni nne.
Kati ya wakazi kuna vikundi vitatu vinavyotofautiana kiutamaduni na kidini: Wabosnia (48%), Waserbia (37.1%) na Wakroatia (14.3%). Wanadai ya kwamba lugha zao ni tofauti, lakini hali halisi ni lugha ileile ya Kislavoni. Wakati wa Yugoslavia iliitwa "Kiserbokroatia". Tofauti ziko kwa sababu Wabosnia hutazamiwa kuwa Waislamu, Waserbia kuwa Waorthodoksi na Wakroatia kuwa Wakristo Wakatoliki.
Nchi ina vitengo viwili: Shirikisho la Bosnia na Herzegovina linalounganisha maeneo ya Waislamu na ya Wakatoliki na Republika Srpska au eneo la Waserbia Waorthodoksi.