Baha'i
From Wikipedia, the free encyclopedia
Imani ya Bahá'í (kwa Kiparsi |بهائی.) ni dini inayofundisha kuabudu Mungu pekee.
Mwanzilishi wake alikuwa Baha'ullah huko Uajemi, (leo Iran) katika karne ya 19, aliyesisitiza umoja wa kiroho wa binadamu wote.[1]
Leo wafuasi wa dini hiyo duniani kote ni kati ya milioni 5 na 6.[2][3]
Katika imani ya Bahá'í, historia inatazamwa kama mfululizo wa wajumbe wa Mungu walioanzisha dini mbalimbali kadiri ya mahitaji ya wakati na watu. Kati yao kuna Abrahamu, Buddha, Yesu, Muhammad na wengineo.
Hatimaye walitokea Báb na Bahá'u'lláh kukamilisha yote ili kuleta amani, haki na umoja.[4]